Skip to main content

Posts

Showing posts from February 13, 2011

Niambie

Naja kwa jina lake Mungu Kwamba yalo moyoni mwangu Yaliyo tamu na machungu Uje kulimuka mwenzangu Ukituliana nikwambie Nitasema pasi kificha Nikuonye bila kukucha Kuwa jambo ‘kikufikicha La ukweli uliochacha Nihisani uniambie Hakuna aliyenyooka Muenda asiyeteguka Kwa wazo au kutamuka Miye pia wakupunguka Ukiona ila nambie Ni wa chira asoonyeka Muambae asokanyika Mara tatu hajaambika Atajuta akikutika Zamu yako ni umwambie kweli mchungu huuma Na hugharimu kuusema Ela ni dawa ya hatima Huja kuuponya mtima Ukiwa nao we’nambie Kanyo lako ukichelea Ukiniona nakosea Kwa Mungu ukijitetea Hesabu utanitolea Kujitoa ila,nambie Niambie liwapo chungu Usinifumbie mizungu Walau likawe uchengu Mwanga wa maozi yangu Usiche kuindha nambie