Skip to main content

Posts

Showing posts from September 1, 2013

Wangu Laazizi!

Wangu Laazizi Ulivyojisabilia, kwangu pasi samahani, Hujakosa kuniwia, radhi nili makosani, na skomi kujivunia, kuwa nawe maishani Mbuya wangu laazizi   Rahimu kanijalia, uwe wangu wa ubani, kito nisichokilalia, kwangu ili hisani Mola kaniumbia, uwe wangu muhisani, Mbuya wangu   laazizi Mara nikikuwaza, nyemi hinija moyoni, nafsi   hukaramukia, ninapokutia matoni pamwe nawe sjajutia, wala nsaili kwa nini Mbuya wangu laazizi   Na wajapotuchimbia, bado hatubandukani, Mawi walotutakia, na tabu zilosakini Yao hukuyasikia, ila uliniamini Mbuya wangu laazizi Mangapi umepitia, kunipenda maskini Lufufu mevumilia, huba letu kudhamini Vya mwiku umejilia, ukinipa na tumaini Mbuya wangu laazizi! Amwali hijitakia, ela uweja fulani Wala raha kupania, kuishi utukufuni Sakafu lijilalia, kusimisutu laini, Mbuya wangu Laazizi!   Pukute ulijilia, hukukimwa majani Sima ulibugia, mchana hata jioni Chai kavu