Skip to main content

Posts

Showing posts from January 2, 2011

Moyo upendao

Moyo wenye kupendao, tena haumilikiwi Hauwi wa apendao, wala maliye hauwi Humwendea apendwao, ukabakia kiziwi Moyo wenye kupendao, na subira hauwi Penzi huutiya mbio, ukawa katu hutuwi Kajikosa mmilikio, ‘kijaribu hatuliwi Kutuza kama atakao, hiariye haiwi Moyo wenye kupendao, na subira hauwi Huwashinda watu sao, una nguvuna kawi Ukawatoka ndanio, kwendeya ajinawi Ukawashinda nafsio, kawa haurudiwi Moyo wenye kupendao, na subira hauwi Ngajaribu wamilikio, kimiani hutiwi Unawatinga uchao, kichele hawatuliwi Penzi liupaniao, ni muzungu hujibiwi Moyo wenye kupendao,na subira hauwi Kama sivyo nisemao, mbona mja hambiwi, Akaziacha na mbio, kageuka ja kiziwi Akapuza waasao, na simile haambiwi Moyo wenye kupendao,na subira hauwi