Skip to main content

Posts

Showing posts from September 5, 2010

Sipendi kucheka

Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali Stendi unipe hidaya sipendi kutenda hili             Sipendi mimi kucheka Sipendi mimi kucheka, kuchekea mawi Sipendi na ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika             Halafuye nikacheka! Masikini akiteswa Yatima akinyanyaswa Mnyonge naye akinyonywa Sipendi hata ikiwa Unazonguvu najuwa Na hili sitatekezwa Mbona lakini nicheke, kwayo furaha? Na wewe ukajiweke, uli na siha? Na yatima ali pweke, wa anahaha? Amenyimwa haki yake, hanayo raha! Na moyo wangu ucheke, kwa ha,ha,ha! Kucheka kwa kucheka Mimi katu sitacheka

sipendi kupayuka

Sikupendi kupayuka, ila leo ninatamka Mlokole n'tasikika, bure sipendi 'payuka Mtima ukisalitika, kusema utataka ukaweze kusikika, bure sipendi payuka Ni huba limeuteka, kawa umesalitika bakunja limeuteka bure sipendi payuka Ndio kunadi 'kataka kote wanikasikika mie men'teka haraka bure sipendi payuka

Mwana nakuasa

Leo nimekuita mwana, Nikupe yangu ya moyo Kwa upole nitanena ‘Kayatiye masikiyo Tabiya hii yako mwana Si yetu tujuwayo Uli wa kulaza damu Na uzembe uzidiyo Pahala nawe hudumu Uchao ni mbiyombiyo Hutufai nawe humu Na hiyo shambiroyo Wapendani naumi Unaiizia gange Hulimi na walimi Wataka ukajitenge Haya sijaona mimi Nakuasa ujichunge Mwiza kazi yu wa chira Ni aendewaye tenge Asiyetaka ajira Wala hashiki shilange Ndiye muja wa hasara Hubomoa asijenge Unavitaka vya bure Hulitoi jasho lako Lako ndizo hamrere Umebaki wa mitiko Uchao ‘wa’tuza bure Sizo zetu nyendo zako La mno lako ni ung’are Uzirembe nyele zako Uturi ujirashire Ukatembee kwa deko Hukosi kuzua ghere Na marashi ya mnuko Unazani utaoa? Utamwoa wa nani? Jasho nalo hujatoa, Utachokishika nini? Utaithibiti ndoa? Wa kukubali nani? Unafaa kujitoa, Fanye kazi kwa manani Na mali ukayazoa Hamadi kibindoni Ndipo utapopoa Ukamtafute mwendani S

Mwana nakuasa

Leo nimekuita mwana, Nikupe yangu ya moyo Kwa upole nitanena ‘Kayatiye masikiyo Tabiya hii yako mwana Si yetu tujuwayo Uli wa kulaza damu Na uzembe uzidiyo Pahala nawe hudumu Uchao ni mbiyombiyo Hutufai nawe humu Na hiyo shambiroyo Wapendani naumi Unaiizia gange Hulimi na walimi Wataka ukajitenge Haya sijaona mimi Nakuasa ujichunge Mwiza kazi yu wa chira Ni aendewaye tenge Asiyetaka ajira Wala hashiki shilange Ndiye muja wa hasara Hubomoa asijenge Unavitaka vya bure Hulitoi jasho lako Lako ndizo hamrere Umebaki wa mitiko Uchao ‘wa’tuza bure Sizo zetu nyendo zako La mno lako ni ung’are Uzirembe nyele zako Uturi ujirashire Ukatembee kwa deko Hukosi kuzua ghere Na marashi ya mnuko Unazani utaoa? Utamwoa wa nani? Jasho nalo hujatoa, Utachokishika nini? Utaithibiti ndoa? Wa kukubali nani? Unafaa kujitoa, Fanye kazi kwa manani Na mali ukayazoa Hamadi kibindoni Ndipo utapopoa Ukamtafute mwendani Si mambo ya kutanga Fi na huyu fi na

Asiye nacho hanacho

Asiye nacho hanacho, hanacho cha kutaja, Kutaja kiitikacho, kiitikacho na mkikaja Kikaja na kilicho, kilicho chenye faraja Faraja tu hanacho, hanacho huyo mja Mja wa kicho hanacho, hanacho ila ana Ja’ Jalali mwenye jaala, jaala ilo ya kheri, Kheri njema na fadhila, fadhila na mstakabali, Mstakabali uso dhila, dhila wala nayo shari, Shari amemkomela, amemkomela dahari Dahari amemfadhila, amemfadhila Jabari Jabari urithi wake, wake yule fakiri Fakiri basi simcheke, simcheke na ghururi, Ghururi haifai kwake, kwake japo hakung’ari, Hakung’ari na vyake, vyake vilivyo dhahiri, Dhahiri usimcheke, usimcheke upate shari, Shari takuta fulani, fulani msahaulifu, Msahulifu wa kanuni, kanuni na wadilifu Wadilifu wa Manani, Manani mwenye kukifu, Kukifu akakuhini, akakuhini mpujufu, Mpujufu msihisani, hisani kwa wapungufu Wapungufu si wa moyo, moyo wanao tele, Tele imani wanayo, wanayo na simile, Simile iwongozayo, iwongozayo milele Milele ‘na kimbiliyo, kimbiliyo la waele