Skip to main content

Posts

Showing posts from August 29, 2010

Arudhi ndio ushairi

Faradhi leo n’kasema, nikapasue mbarika asilani sitonyama’, kinaganaga ntatamka nikosoe alosema, yake malenga wa nyika Unisikize kwa wema, lau uje utalimka Walau utalimuka, ukajue la kusema Ushairi si kutamka,unagharimu taluma Si majambo kuweka, na watu kuyasoma Tungo zinayo mipaka, na ufundi wa kufuma Ufundi wa kuzifuma, kwa vina muafaka Kuviweka na vya ngama’, na tamati ukifika Viwe na urari mwema, na utamu wa kusomeka Msuko na mandhuma, usita na kadhalika Si mwisho kadhalika, kuna nyingi nikusema Mtiririko kutirika, ‘sita na kifunganyama Ndo tungo  za kusomeka, si zile unazosema Arudhi ni ufundi kaka, wa kwongoa na mtima Kuuongoa mtima, lazima kumakinika Kubambanya si kwema, tungo ukiziandika Vue ni  ja kuangema, kuchelea kwajibika Na kwogopa gharama, na mwia wa kuandika

mtu hafi kupenda

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

uketo wa sanaa ya ushairi

huduma za kijamii

Tatasi za mtima

Kama unamjua jamani, Kanisailie kwa nini Mbona na mimi haneni, na mwendoye sina sinani Nachotaka ni hisani, walahi sina kisirani Nataka awe mwendani, iwapo n'tapawa idhini Zangu n’tetesi za mtima, zan’tatiza hadi kusema zanipa nyingi nakama, na kupoka yangu naima Anavyofanya si vyema, kamuelezeni kwa hima Kwamba ninaaengema, na inaniisha neema Kama ujumbe metuma, ni kama kadinda kusoma Kama sivyo angesema, pengine naye akatuma Kwa tuo ningesoma, niyajue anayosema Nijue kama ni kwema, ‘kajiamulie mapema Nimeamba yote Nzisa, sinayo mengine kwa sasa lau kije kuwa kisa, niliyemtaka nikakosa Wala sinambe siasa, ninaatilika kabisa Ukimuona angusa, na usiipoteze ruksa Umwambie aitike, si vyema akaniteleke, Kwenye laini umweke, ulainishe moyo wake Macho yake afunguke, na mtima wake uamke Akubali miye wake, aliye laazizi wake N’ mema yenu maitiko, ni heri kusema kuliko Ila hayan’tui mtwiko, wala yakanipa kiteko Kan’tafutie aliko, kamweleze hapa niliko Sinacho mimi kicheko, ni machoz