Skip to main content

Posts

Showing posts from November 27, 2011

vingawa vyaliwa

Vingine kama kuliwa,vinono na vitamu Vinywewa au tafunwa,vinavyokutia hamu A cha hata ungapawa, viwavyo navyo haramu Vitu vingawa vyaliwa, halali ndivyo muhimu Vingine kama vyaliwa, uindhari binadamu, Vingine havitaliwa, visikuletee hukumu Ulapo vikaliliwa, vitakugeuka sumu Vitu vingawa vyaliwa, halali ndivyo muhimu Vingine kama vyaliwa, punguza yako hamumu, Visiwe vinyang’anywa, gharama yake ni ngumu Vingapo hata kufichwa, kamwe navyo havidumu Vitu vingawa vyaliwa, halali ndivyo muhimu Vingine kama vyaliwa, vingine kwa utalamu, Vikawa havitambuwa, ashaona Mungu Karimu, Hakika vitatapikwa, peupe mbe’ ya kaumu Vitu vingawa vyaliwa, halali ndivyo muhimu Wamalwa Kevin Mlokole Mulumbi FLTA alumni 2010/2011