Skip to main content

Posts

Showing posts from January 9, 2011

Waziri

Nina hili la kujua, mkaniwekee dhahiri, Utata mkautatua, mkanipeni na fasiri Ni jambo la nisumbua, lanikiera kifikiri Anacho nini waziri, au waziri ni wa-siri? Ni nini amekificha, kama waziri ni wa-siri? Nini anachokicha, asijiweke dhahiri? Wazimu umemchacha, kawa wakutofikiri? Augua nini waziri, au ana bawasiri? Mbona hana razini, ‘wapo hana bawasiri? Mbona yeye hatuoni, madhila yamekithiri! Anatutiya shimoni, mwa madhila na shari Waziri kweli waziri, au yeye wa-aziri? Amepania hakomi, kusitisha athari, Zimezidi mara kumi, athari za ubepari, Anajinaki ni msomi, kwetu siye ajibari Kujua mie nashindwa, ni waziri au hasiri? Ni nani wahasiriwa, awapo yeye hasiri? Wewe usiye jaliwa, mja usiye na kheri Mimi nisiyejengewa, Kama hilo lake kasri Ni wewe na mimi yakhe, tunaopata athari Basi kazi yake nini, anayotenda waziri? Au kutamba garini, akienda nyigi ziari Kwenda mahotelini, na kulewa chakari, Nijibu anani waziri, achofanya barazani