Skip to main content

Posts

Showing posts from January 6, 2013
Hajafua Dafu Kama alivyo msasi, endaye kuwinda huwa Jenda kwa hamu na kasi,  kilenga kunasa njiwa Zimpatapo khasaisi, kumbe ndege hakutuwa Bado dafu hajafuwa, Mdavadi kijita Mesi Kwa makeke kahujuru, kuitafuta muruwa, Aionje hewa huru, kumbe nako  haikuwa Akapunjwa na Uhuru, alotaka kahiniwa Kabaki mechachamuwa,   zimwishiye furufuru Lisadiki sakumbimbi, walomlisha vongono  Kapotoshwa na wachimbi, na waja wasimaono Kamtowa kwenye kambi, alikopata usono Sasa yuasaga meno, akiulizwa haambi Kendea virambaramba, vichicha vya ukoloni Ndio navyo yuagamba, kuwa farasi mbioni Ni kama guo la mtumba, ‘pambwe mwari arusini Hata hawiki mjini, KANU jogoo wa shamba Nakoma wasiniambe, wanitusi wajuao Nachelea wanichimbe, wan’dhuru vibarakao Ila n’metowa ujumbe, wamwindhe nahodha wao “Sijetuwa meli yao, kwenye kaburi chimbe K.W Wamalwa Mlokole Mlumbi Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison