Skip to main content

Posts

Showing posts from April 3, 2011

karama

Siendi Kinyumenyume Siendi kinyumenyume kama mshamba wa kimeme Ndoto yanitia shime Japo nagwa nisimame Nikatwete na niheme N'takakania kiume Nikaziangushe ngome Na, Nitasongesha milima Ndiani ilosimama Nitashinda wanonizima Wanonifisha na mtima Nitafika hata kama Nuru zote zimezima Nacho kiza kusakama Nitaifikia yangu karama

Uniambae!

Kama utanisikiya, nambe haya kukuindha Majambo nilowaziya, si moja ila ni kadha Yenye heri kufaidiya, ungayafwata faradha Kama sivyo swahibiya, kanikome unambae Kama uli wa kukimbiya, na haraka za vitendo, Naona huton’faiya, zangu ni za pole nyendo Mambo mi’ hiyapaniya, haraka ina uvundo Kama hutosubiriya, unikome uniambae Kama limi umenoya, linakata kama msu Na Inda kutapakaya, ndugu kuwagawa nusu Nyoyo kuwakereya, na kukeeza ja kisu Kama ndugu kuchukiya, unikome uniambae