Skip to main content

Posts

Showing posts from March 20, 2011

Siku ya Ulifi

Toka Hegi yasikika, imelia parapanda Wafike walotajika, wasilimatie kwenda Majina waliandika, na ila walizotenda Waache kuhemeka, ili siku ya ulifi Nawaasa wahusika, waziache propaganda Hifai kulalamika, kila wanakokuenda Wengine tope kupaka, jukwaani wakipanda Wakuache kupayuka, ili siku ya ulifi Wenyewe waliyataka, mbegu mbaya walipanda Na chuki waliipika, ikaiva na kuvunda Na Umma ukagawika, maovu ukajitenda Sasa wana jakajaka, ili siku ya ulifi Mahuluki bila shaka, huvuna ‘lichopanda Na maji ukiyateka, uyanywe yote mafunda Na koo ikikabika, shauriyo ‘liyaenda Ela watawajibika, ili siku ya ulifi Wacheni kutikatika, kotekote mukiranda Mwakutaka kusifika, wafuasi mwawawinda Mwashinda kunung’unika, na mambo munayapinda Ishara ya kutishika, ili siku ya Ulifi Kama ni kutakasika, ni heri mkatuenenda Ghofira mkatutaka, tukawapa tukipenda Mumwombe Mahuluka, faraja akawatenda Badala ya kutimuka, ili siku ya ulifi Hitaaihirishika, siku ya ndege kupanda Mkayajibu mashtaka, ya zenu ila