Wangu Laazizi Ulivyojisabilia, kwangu pasi samahani, Hujakosa kuniwia, radhi nili makosani, na skomi kujivunia, kuwa nawe maishani Mbuya wangu laazizi Rahimu kanijalia, uwe wangu wa ubani, kito nisichokilalia, kwangu ili hisani Mola kaniumbia, uwe wangu muhisani, Mbuya wangu laazizi Mara nikikuwaza, nyemi hinija moyoni, nafsi hukaramukia, ninapokutia matoni pamwe nawe sjajutia, wala nsaili kwa nini Mbuya wangu laazizi Na wajapotuchimbia, bado hatubandukani, Mawi walotutakia, na tabu zilosakini Yao hukuyasikia, ila uliniamini Mbuya wangu laazizi Mangapi umepitia, kunipenda maskini Lufufu mevumilia, huba letu kudhamini Vya mwiku umejilia, ukinipa na tumaini Mbuya wangu laazizi! Amwali hijitakia, ela uweja fulani Wala raha kupania, kuishi utukufuni Sakafu lijilalia, kusimisutu laini, Mbuya wangu Laazizi! Pukute ulijilia, hukukimwa majani Sima ulibugia, mchana hata jioni Chai kavu
Ukumbi huu unalenga kukupa uhondo wa sanaa ya ushairiwa kiswahili. utapata mashairi mengi ambayo nimeyatunga mwenye na mengine yakachapisha kwenye Taifa Leo. Kando na haya utapata kufaidika na makala ya kukuhimiza ikiwa wewe ni mkrsito. Yamkini nitalenga kuwakidhia mahitaji mbalimbali ya kukujengeni. ****** Get entertained with lots of Swahili poems posted daily. Watch movies by going to "movies!!! button. Lots of Items to buy instantly at "Nunua/Buy Items" page and Lots of other good deals!