Moyo wenye kupendao, tena haumilikiwi
Hauwi wa apendao, wala maliye hauwi
Humwendea apendwao, ukabakia kiziwi
Moyo wenye kupendao, na subira hauwi
Penzi huutiya mbio, ukawa katu hutuwi
Kajikosa mmilikio, ‘kijaribu hatuliwi
Kutuza kama atakao, hiariye haiwi
Moyo wenye kupendao, na subira hauwi
Huwashinda watu sao, una nguvuna kawi
Ukawatoka ndanio, kwendeya ajinawi
Ukawashinda nafsio, kawa haurudiwi
Moyo wenye kupendao, na subira hauwi
Ngajaribu wamilikio, kimiani hutiwi
Unawatinga uchao, kichele hawatuliwi
Penzi liupaniao, ni muzungu hujibiwi
Moyo wenye kupendao,na subira hauwi
Kama sivyo nisemao, mbona mja hambiwi,
Akaziacha na mbio, kageuka ja kiziwi
Akapuza waasao, na simile haambiwi
Moyo wenye kupendao,na subira hauwi
Hauwi wa apendao, wala maliye hauwi
Humwendea apendwao, ukabakia kiziwi
Moyo wenye kupendao, na subira hauwi
Penzi huutiya mbio, ukawa katu hutuwi
Kajikosa mmilikio, ‘kijaribu hatuliwi
Kutuza kama atakao, hiariye haiwi
Moyo wenye kupendao, na subira hauwi
Huwashinda watu sao, una nguvuna kawi
Ukawatoka ndanio, kwendeya ajinawi
Ukawashinda nafsio, kawa haurudiwi
Moyo wenye kupendao, na subira hauwi
Ngajaribu wamilikio, kimiani hutiwi
Unawatinga uchao, kichele hawatuliwi
Penzi liupaniao, ni muzungu hujibiwi
Moyo wenye kupendao,na subira hauwi
Kama sivyo nisemao, mbona mja hambiwi,
Akaziacha na mbio, kageuka ja kiziwi
Akapuza waasao, na simile haambiwi
Moyo wenye kupendao,na subira hauwi
Comments