Skip to main content

Waziri

Nina hili la kujua, mkaniwekee dhahiri,
Utata mkautatua, mkanipeni na fasiri
Ni jambo la nisumbua, lanikiera kifikiri
Anacho nini waziri, au waziri ni wa-siri?

Ni nini amekificha, kama waziri ni wa-siri?
Nini anachokicha, asijiweke dhahiri?
Wazimu umemchacha, kawa wakutofikiri?
Augua nini waziri, au ana bawasiri?

Mbona hana razini, ‘wapo hana bawasiri?
Mbona yeye hatuoni, madhila yamekithiri!
Anatutiya shimoni, mwa madhila na shari
Waziri kweli waziri, au yeye wa-aziri?

Amepania hakomi, kusitisha athari,
Zimezidi mara kumi, athari za ubepari,
Anajinaki ni msomi, kwetu siye ajibari
Kujua mie nashindwa, ni waziri au hasiri?

Ni nani wahasiriwa, awapo yeye hasiri?
Wewe usiye jaliwa, mja usiye na kheri
Mimi nisiyejengewa, Kama hilo lake kasri
Ni wewe na mimi yakhe, tunaopata athari

Basi kazi yake nini, anayotenda waziri?
Au kutamba garini, akienda nyigi ziari
Kwenda mahotelini, na kulewa chakari,
Nijibu anani waziri, achofanya barazani

Comments

Popular posts from this blog

Mja hafi kupenda

Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Yupi mwenye haki

1.           Yupi ale mahuluki, asiye kuwa na doa Ni yupi ale na haki, asiye wa kukosoa Mja ambaye hakiuki, akawa wa kupotea Hayupo muenye haki, maki wote meondoa 2.           Yupi asiye wa kosa, mnyofu wazo nyendo, Awapo aseme sasa, akajinegee kando, Yule ale jitakasa, safi hanao uvundo Hakuna asiyekosa, kwa kauli na matendo 3.           Sijaona aliyejitosha, akahimili nafsiye Insi asejikunguisha, ulimi kwa kauliye Nani asiye keresha, kubughudhi muumbaye Ila tu akajikosha, akatubia dhambiye 4.           Nani asiyekunguwaa, kwa fikra ya moyoni Kunaye asiye na waa, lilofichama wazoni? Awe mja anayefaa, kwa Rabana machoni? Wote wamepunguwaa, utukufu hawaoni.   5.           Yupi basi wa kupona? amchaye Mola wake Nani ataka...