Skip to main content

Hajafua Dafu
Kama alivyo msasi, endaye kuwinda huwa
Jenda kwa hamu na kasi,  kilenga kunasa njiwa
Zimpatapo khasaisi, kumbe ndege hakutuwa
Bado dafu hajafuwa, Mdavadi kijita Mesi

Kwa makeke kahujuru, kuitafuta muruwa,
Aionje hewa huru, kumbe nako  haikuwa
Akapunjwa na Uhuru, alotaka kahiniwa
Kabaki mechachamuwa,   zimwishiye furufuru

Lisadiki sakumbimbi, walomlisha vongono
 Kapotoshwa na wachimbi, na waja wasimaono
Kamtowa kwenye kambi, alikopata usono
Sasa yuasaga meno, akiulizwa haambi

Kendea virambaramba, vichicha vya ukoloni
Ndio navyo yuagamba, kuwa farasi mbioni
Ni kama guo la mtumba, ‘pambwe mwari arusini
Hata hawiki mjini, KANU jogoo wa shamba

Nakoma wasiniambe, wanitusi wajuao
Nachelea wanichimbe, wan’dhuru vibarakao
Ila n’metowa ujumbe, wamwindhe nahodha wao
“Sijetuwa meli yao, kwenye kaburi chimbe

K.W Wamalwa
Mlokole Mlumbi
Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison

Comments

Popular posts from this blog

Mja hafi kupenda

Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Yupi mwenye haki

1.           Yupi ale mahuluki, asiye kuwa na doa Ni yupi ale na haki, asiye wa kukosoa Mja ambaye hakiuki, akawa wa kupotea Hayupo muenye haki, maki wote meondoa 2.           Yupi asiye wa kosa, mnyofu wazo nyendo, Awapo aseme sasa, akajinegee kando, Yule ale jitakasa, safi hanao uvundo Hakuna asiyekosa, kwa kauli na matendo 3.           Sijaona aliyejitosha, akahimili nafsiye Insi asejikunguisha, ulimi kwa kauliye Nani asiye keresha, kubughudhi muumbaye Ila tu akajikosha, akatubia dhambiye 4.           Nani asiyekunguwaa, kwa fikra ya moyoni Kunaye asiye na waa, lilofichama wazoni? Awe mja anayefaa, kwa Rabana machoni? Wote wamepunguwaa, utukufu hawaoni.   5.           Yupi basi wa kupona? amchaye Mola wake Nani ataka...