Skip to main content

Wangu Laazizi!


Wangu Laazizi

Ulivyojisabilia, kwangu pasi samahani,

Hujakosa kuniwia, radhi nili makosani,

na skomi kujivunia, kuwa nawe maishani

Mbuya wangu laazizi

 
Rahimu kanijalia, uwe wangu wa ubani,

kito nisichokilalia, kwangu ili hisani

Mola kaniumbia, uwe wangu muhisani,

Mbuya wangu  laazizi


Mara nikikuwaza, nyemi hinija moyoni,

nafsi  hukaramukia, ninapokutia matoni

pamwe nawe sjajutia, wala nsaili kwa nini

Mbuya wangu laazizi

 
Na wajapotuchimbia, bado hatubandukani,

Mawi walotutakia, na tabu zilosakini

Yao hukuyasikia, ila uliniamini

Mbuya wangu laazizi


Mangapi umepitia, kunipenda maskini

Lufufu mevumilia, huba letu kudhamini

Vya mwiku umejilia, ukinipa na tumaini

Mbuya wangu laazizi!


Amwali hijitakia, ela uweja fulani

Wala raha kupania, kuishi utukufuni

Sakafu lijilalia, kusimisutu laini,

Mbuya wangu Laazizi!

 

Pukute ulijilia, hukukimwa majani

Sima ulibugia, mchana hata jioni

Chai kavu lijinywia, hukuuliza jibini

Mbuya wangu Laazizi!


Mlokole
 

 

Comments

Popular posts from this blog

Samehe usamehewe

Hayupo mja duniani asiyekosa asilani wala asitake samahani na imani ya mwenziwe Awe ndugu awe dada, au mwana.. Basi… kama hayupo asiyekosa akaitaka ghufira madhambiye kuondowa na , kwonewa imani na rehema, akawekwe huru nafsiye awe baba au mamaye binti au rafiki Basi, kwake kusahe ni faradhi mja mwene ila, samehe usamehewe Mlokole Mlumbi

uketo wa sanaa ya ushairi

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye