Skip to main content

Waziri

Nina hili la kujua, mkaniwekee dhahiri,
Utata mkautatua, mkanipeni na fasiri
Ni jambo la nisumbua, lanikiera kifikiri
Anacho nini waziri, au waziri ni wa-siri?

Ni nini amekificha, kama waziri ni wa-siri?
Nini anachokicha, asijiweke dhahiri?
Wazimu umemchacha, kawa wakutofikiri?
Augua nini waziri, au ana bawasiri?

Mbona hana razini, ‘wapo hana bawasiri?
Mbona yeye hatuoni, madhila yamekithiri!
Anatutiya shimoni, mwa madhila na shari
Waziri kweli waziri, au yeye wa-aziri?

Amepania hakomi, kusitisha athari,
Zimezidi mara kumi, athari za ubepari,
Anajinaki ni msomi, kwetu siye ajibari
Kujua mie nashindwa, ni waziri au hasiri?

Ni nani wahasiriwa, awapo yeye hasiri?
Wewe usiye jaliwa, mja usiye na kheri
Mimi nisiyejengewa, Kama hilo lake kasri
Ni wewe na mimi yakhe, tunaopata athari

Basi kazi yake nini, anayotenda waziri?
Au kutamba garini, akienda nyigi ziari
Kwenda mahotelini, na kulewa chakari,
Nijibu anani waziri, achofanya barazani

Comments

Popular posts from this blog

Ningekwambia!

Kama ingekuwa vile, swahiba ningeshasema Ningepiga na kelele, ufahamu himahima Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima Ningejasiri n’kwambie, lau sikupendi mbuya Kama sivyo ‘ngekwambiya, wazi wazi pasi siri Lau sijasuhubiya, nahari sikufikiri Kwamba sijakuwaziya, na gonezi kuabiri Ngaungama wangu mwari, kwamba siwe nimpendaye Kama kuli mwengineye, ninaye muenendea Mtimangu anitwaliye, ni radhi kumwenendea Hadhi yangu nimpaye, na siwe wangu maridia Ngakwambia siweye, hala ningekuhubiri Kama siwe ulinitwaa, kawa wa kunipa tuo Najenenda nili fwaa, nimetekwa na pumbao Azizi u’vyonivaa, yakaniisha matao Kweli ningeshakujuza, kwamba siwe nyonda

mtu hafi kupenda

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

penzi

penzi la kulazimisha,lina gharama, kando na kukalifisha, linakukama, na linakufilisisha, likakukwama, hadi likakubakisha, u litima aimi nakujulisha, uwe salama usipende kujishasha, na kwa lazima penda anorejesha, nayo kheshima huba ja hili hukosha, wako mtima ... mbwene hoa walopenda, kwa kusukuma, hatimaye zao zanda, wakaziuma, kumbe hao walopenda, wamewahama amwalio zimeenda, sa' wamezama