Skip to main content

Kukrani!



Shukrani!
Shukrani zangu jazila, kwa chama cha NCOLTCL (nikotiko)
Akawajazi jaala, kwa kutupa mualiko
Tumeteremea kulla, tulosoma toka kwako
Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha

Sikomi kuwahongera, walimu walofundisha
walivyojifunga nira, ya maarifa kutupasha
Tuzijenge mbinu bora, Kiswahili kufundisha
Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha

Mambo hayo ni muhimu, mlotupasha uchao
Mliyeshusha magumu, ya nadharia zao
Tuboreke walimu, kwa wale tufudnishao
Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha

Hongera mwalimu Kiarie, kwa kuonyesha mifano
Lisanza nikusifie, kwazo sifa nono nono
Alwiya zikufikie, ulivyokuwa mfano
Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha

Sikusahau Atonia, kwa wako ukakamavu,
Jinsi ulokakania, pasi kuonya ochovu
Uneemee dunia, kwa kutupa wangavu
Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha

Wanafunzi mlofika, shukrani nyingi sana
Kwenu kuwa washirika, na mwiya wenu kupana
Na sisi tukazoeka, na vipindi vilofana
Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha

Hongera Kesi, Kartika, na Melisa kwayo ari
Chelisi ulisikika, kwa ari na machachari
Nelisoni naye Jaka (jack), pongezi kwa uhodari
Sasa mmelishamuka, na mbinu kujifundisha

Nafasi hiniruhusu, nikawataje kwa jina
Ingehalali kwa busu, ningewapa tangu jana
Silasi upate nusu, kisha nimpe Diana
Kwani tumeshalimuka, na mbinu kujifundisha

Kwaheri ya kuonana, kirejea viamboni
Awatunze Maulana, tutaonana usoni
Na ari tumepashana, tuzidi kuikokeni
Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha

©Mlokole Mlumbi
Kevin Wamalwa
Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison

Comments

Popular posts from this blog

Samehe usamehewe

Hayupo mja duniani asiyekosa asilani wala asitake samahani na imani ya mwenziwe Awe ndugu awe dada, au mwana.. Basi… kama hayupo asiyekosa akaitaka ghufira madhambiye kuondowa na , kwonewa imani na rehema, akawekwe huru nafsiye awe baba au mamaye binti au rafiki Basi, kwake kusahe ni faradhi mja mwene ila, samehe usamehewe Mlokole Mlumbi

uketo wa sanaa ya ushairi

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye