Skip to main content

Kenya Itakuwepo

Niskize kote mlipo, niwape huno ujuzi
Siku ya kura ijapo, ‘kiteuwa viongozi
Kabila zetu zingapo, nyingi baidi ki’zazi
Tutunze kenya iwepo, baada ya uchaguzi

Na siasa tupigapo, tusitiye machokozi,
kila mwahala twendapo, tudhihirishe wongozi,
na wala sio matapo, ya kuzua machukizi,
Hi' kenya itakuwapo, baada ya uchaguzi.

Wazi mwajuwa malipo, ya kuzua uchafuzi,
na kujifanya mapopo, tusiyatie maozi,
ela yatendwe tulipo, wengi kawa wakimbizi,
twataka kenya iwepo, baada ya uchaguzi

kataa vidingapopo, vya kuzua uchochezi
nao hawatakuwapo, tukichomana kwa mionzi
wakipoa kwao pepo, nasi twazipiga kwenzi
tuombe Kenya iwepo, baada ya uchaguzi

Sisemi kupita hapo, menikaba usingizi,
na chini nijilazapo, nawaasa wasikizi,
kila mwahala mlipo, tusirudiye ya juzi,
ili kenya ikawepo, baada ya uchaguzi.

K.W Wamalwa
Mlokole Mlumbi
Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison

Comments

Popular posts from this blog

Mja hafi kupenda

Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Yupi mwenye haki

1.           Yupi ale mahuluki, asiye kuwa na doa Ni yupi ale na haki, asiye wa kukosoa Mja ambaye hakiuki, akawa wa kupotea Hayupo muenye haki, maki wote meondoa 2.           Yupi asiye wa kosa, mnyofu wazo nyendo, Awapo aseme sasa, akajinegee kando, Yule ale jitakasa, safi hanao uvundo Hakuna asiyekosa, kwa kauli na matendo 3.           Sijaona aliyejitosha, akahimili nafsiye Insi asejikunguisha, ulimi kwa kauliye Nani asiye keresha, kubughudhi muumbaye Ila tu akajikosha, akatubia dhambiye 4.           Nani asiyekunguwaa, kwa fikra ya moyoni Kunaye asiye na waa, lilofichama wazoni? Awe mja anayefaa, kwa Rabana machoni? Wote wamepunguwaa, utukufu hawaoni.   5.           Yupi basi wa kupona? amchaye Mola wake Nani ataka...