Toka Hegi yasikika, imelia parapanda
Wafike walotajika, wasilimatie kwenda
Majina waliandika, na ila walizotenda
Waache kuhemeka, ili siku ya ulifi
Nawaasa wahusika, waziache propaganda
Hifai kulalamika, kila wanakokuenda
Wengine tope kupaka, jukwaani wakipanda
Wakuache kupayuka, ili siku ya ulifi
Wenyewe waliyataka, mbegu mbaya walipanda
Na chuki waliipika, ikaiva na kuvunda
Na Umma ukagawika, maovu ukajitenda
Sasa wana jakajaka, ili siku ya ulifi
Mahuluki bila shaka, huvuna ‘lichopanda
Na maji ukiyateka, uyanywe yote mafunda
Na koo ikikabika, shauriyo ‘liyaenda
Ela watawajibika, ili siku ya ulifi
Wacheni kutikatika, kotekote mukiranda
Mwakutaka kusifika, wafuasi mwawawinda
Mwashinda kunung’unika, na mambo munayapinda
Ishara ya kutishika, ili siku ya Ulifi
Kama ni kutakasika, ni heri mkatuenenda
Ghofira mkatutaka, tukawapa tukipenda
Mumwombe Mahuluka, faraja akawatenda
Badala ya kutimuka, ili siku ya ulifi
Hitaaihirishika, siku ya ndege kupanda
Mkayajibu mashtaka, ya zenu ila na inda
Nyoyo na zikaponyeka, na makovu yalovunda
Haki itapofanyika, ili siku ya ulifi
Kevin wamalwa
Mlokole Mlumbi
Chuo Kikuu cha Bluefield state,
Marekani
Comments