Skip to main content

Ukila

Ukila kile kichakwe, cha mwenzio usile
Ukila wa pupa ‘siwe, pupa nayo ni ndwele
Ukila haramu s’tukue, cha mwendo sikitwale
Ukila nla halali ‘we, cha chira na usile

Usile waja kuamba, ‘kawa kauli nawe
Usile ukajigamba, kukila kisichakwe
Usile na kwa mafamba, litoe jasho lakwe
Usile wala kuramba, na cha hila kisiliwe

Kisiliwe cha litima, wasio na uwezo
Kisiliwe cha yatima, chao wastahilizo
Kisiliwe hata kama, wewe una uwezo
Kisiliwe na cha umma, tatapika ulazo

Ulazo na kwa ghiliba, huwa sumu mwenzangu,
Ulazo na ukashiba, utalipa kwa Mungu
Ulazo ziwezo baba, fedha za mwendo chungu
Ulazo hata zi’haba, ziwe zako ndu’yangu

Comments

Popular posts from this blog

Bin-Adamu

Mimi Natakadamu ino nudhumu Nikayaambe yalomuhimu Yanotaja ghilba za bin-Adamu Wa kuhalalisha yalokharamu kufaidi yake tamaa na hamumu Yalo mema kayatiya sumu Na kuwaseta walomaamumu Wakijigeuza sanamu Wakisahau wali wanadamu Kataka ibada kwa kaumu Wadhani Takwepa luhdi wakisha humu Watakinza ya Mungu Kalamu Kwamba Muhuluku hafahamu ati hiyeyuki fuadi ngumu Ila Wendelepi siku ya hukumu? Watapokwima mbele ya Hakimu Kulipiya wao udhalimu Kama si nyoto za Jehanamu? Zitakao waunguza kwa zamu Zikisha lamba mifupa na damu Watauma zanda na kujilaumu kwa wao utimamu wa wazimu ©Wamalwa

Siku ya Ulifi

Toka Hegi yasikika, imelia parapanda Wafike walotajika, wasilimatie kwenda Majina waliandika, na ila walizotenda Waache kuhemeka, ili siku ya ulifi Nawaasa wahusika, waziache propaganda Hifai kulalamika, kila wanakokuenda Wengine tope kupaka, jukwaani wakipanda Wakuache kupayuka, ili siku ya ulifi Wenyewe waliyataka, mbegu mbaya walipanda Na chuki waliipika, ikaiva na kuvunda Na Umma ukagawika, maovu ukajitenda Sasa wana jakajaka, ili siku ya ulifi Mahuluki bila shaka, huvuna ‘lichopanda Na maji ukiyateka, uyanywe yote mafunda Na koo ikikabika, shauriyo ‘liyaenda Ela watawajibika, ili siku ya ulifi Wacheni kutikatika, kotekote mukiranda Mwakutaka kusifika, wafuasi mwawawinda Mwashinda kunung’unika, na mambo munayapinda Ishara ya kutishika, ili siku ya Ulifi Kama ni kutakasika, ni heri mkatuenenda Ghofira mkatutaka, tukawapa tukipenda Mumwombe Mahuluka, faraja akawatenda Badala ya kutimuka, ili siku ya ulifi Hitaaihirishika, siku ya ndege kupanda Mkayajibu mashtaka, ya zenu ila...