Kama ingekuwa vile, swahiba ningeshasema
Ningepiga na kelele, ufahamu himahima
Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima
Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima
Ningejasiri n’kwambie, lau sikupendi mbuya
Kama sivyo ‘ngekwambiya, wazi wazi pasi siriLau sijasuhubiya, nahari sikufikiri
Kwamba sijakuwaziya, na gonezi kuabiri
Ngaungama wangu mwari, kwamba siwe nimpendaye
Kama kuli mwengineye, ninaye muenendea
Mtimangu anitwaliye, ni radhi kumwenendea
Hadhi yangu nimpaye, na siwe wangu maridia
Ngakwambia siweye, hala ningekuhubiri
Kama siwe ulinitwaa, kawa wa kunipa tuo
Najenenda nili fwaa, nimetekwa na pumbao
Azizi u’vyonivaa, yakaniisha matao
Kweli ningeshakujuza, kwamba siwe nyonda
Comments