Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye
Ukumbi huu unalenga kukupa uhondo wa sanaa ya ushairiwa kiswahili. utapata mashairi mengi ambayo nimeyatunga mwenye na mengine yakachapisha kwenye Taifa Leo. Kando na haya utapata kufaidika na makala ya kukuhimiza ikiwa wewe ni mkrsito. Yamkini nitalenga kuwakidhia mahitaji mbalimbali ya kukujengeni. ****** Get entertained with lots of Swahili poems posted daily. Watch movies by going to "movies!!! button. Lots of Items to buy instantly at "Nunua/Buy Items" page and Lots of other good deals!
Comments