Skip to main content

Yupi mwenye haki


1.          Yupi ale mahuluki, asiye kuwa na doa
Ni yupi ale na haki, asiye wa kukosoa
Mja ambaye hakiuki, akawa wa kupotea
Hayupo muenye haki, maki wote meondoa

2.          Yupi asiye wa kosa, mnyofu wazo nyendo,
Awapo aseme sasa, akajinegee kando,
Yule ale jitakasa, safi hanao uvundo
Hakuna asiyekosa, kwa kauli na matendo

3.          Sijaona aliyejitosha, akahimili nafsiye
Insi asejikunguisha, ulimi kwa kauliye
Nani asiye keresha, kubughudhi muumbaye
Ila tu akajikosha, akatubia dhambiye

4.          Nani asiyekunguwaa, kwa fikra ya moyoni
Kunaye asiye na waa, lilofichama wazoni?
Awe mja anayefaa, kwa Rabana machoni?
Wote wamepunguwaa, utukufu hawaoni.
 
5.          Yupi basi wa kupona? amchaye Mola wake
Nani atakayemwona? Asafiye nafsi yake,
Mja yupi atayefana? Aseficha ila zake,
Amwombaye Rabana, njia zake zinyoke

Comments

Popular posts from this blog

Mja hafi kupenda

Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye