Skip to main content

Mja hafi kupenda

Hapana mja duniani, apenda aondowe
Si khiari asilani, rohoye aitowe
Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe
Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye

Ni kudura ya Manani, alompa utuwe
Hana na lake Fulani, sema akohowe
Hanalo la lakini, zake ziandikiwe
Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye        

Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe
Au aishi theneni, neema ajaliwe
Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe
Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye


Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye
Ngebaki duniani, amwali ajiliye
 Afurahi maishani, na wale wampendaye
Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Comments

Popular posts from this blog

Yupi mwenye haki

1.           Yupi ale mahuluki, asiye kuwa na doa Ni yupi ale na haki, asiye wa kukosoa Mja ambaye hakiuki, akawa wa kupotea Hayupo muenye haki, maki wote meondoa 2.           Yupi asiye wa kosa, mnyofu wazo nyendo, Awapo aseme sasa, akajinegee kando, Yule ale jitakasa, safi hanao uvundo Hakuna asiyekosa, kwa kauli na matendo 3.           Sijaona aliyejitosha, akahimili nafsiye Insi asejikunguisha, ulimi kwa kauliye Nani asiye keresha, kubughudhi muumbaye Ila tu akajikosha, akatubia dhambiye 4.           Nani asiyekunguwaa, kwa fikra ya moyoni Kunaye asiye na waa, lilofichama wazoni? Awe mja anayefaa, kwa Rabana machoni? Wote wamepunguwaa, utukufu hawaoni.   5.           Yupi basi wa kupona? amchaye Mola wake Nani ataka...