Skip to main content

Popular posts from this blog

Bin-Adamu

Mimi Natakadamu ino nudhumu Nikayaambe yalomuhimu Yanotaja ghilba za bin-Adamu Wa kuhalalisha yalokharamu kufaidi yake tamaa na hamumu Yalo mema kayatiya sumu Na kuwaseta walomaamumu Wakijigeuza sanamu Wakisahau wali wanadamu Kataka ibada kwa kaumu Wadhani Takwepa luhdi wakisha humu Watakinza ya Mungu Kalamu Kwamba Muhuluku hafahamu ati hiyeyuki fuadi ngumu Ila Wendelepi siku ya hukumu? Watapokwima mbele ya Hakimu Kulipiya wao udhalimu Kama si nyoto za Jehanamu? Zitakao waunguza kwa zamu Zikisha lamba mifupa na damu Watauma zanda na kujilaumu kwa wao utimamu wa wazimu ©Wamalwa

Ukila

Ukila kile kichakwe, cha mwenzio usile Ukila wa pupa ‘siwe, pupa nayo ni ndwele Ukila haramu s’tukue, cha mwendo sikitwale Ukila nla halali ‘we, cha chira na usile Usile waja kuamba, ‘kawa kauli nawe Usile ukajigamba, kukila kisichakwe Usile na kwa mafamba, litoe jasho lakwe Usile wala kuramba, na cha hila kisiliwe Kisiliwe cha litima, wasio na uwezo Kisiliwe cha yatima, chao wastahilizo Kisiliwe hata kama, wewe una uwezo Kisiliwe na cha umma, tatapika ulazo Ulazo na kwa ghiliba, huwa sumu mwenzangu, Ulazo na ukashiba, utalipa kwa Mungu Ulazo ziwezo baba, fedha za mwendo chungu Ulazo hata zi’haba, ziwe zako ndu’yangu

Kukrani!

Shukrani! Shukrani zangu jazila, kwa chama cha NCOLTCL (nikotiko) Akawajazi jaala, kwa kutupa mualiko Tumeteremea kulla, tulosoma toka kwako Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Sikomi kuwahongera, walimu walofundisha walivyojifunga nira, ya maarifa kutupasha Tuzijenge mbinu bora, Kiswahili kufundisha Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Mambo hayo ni muhimu, mlotupasha uchao Mliyeshusha magumu, ya nadharia zao Tuboreke walimu, kwa wale tufudnishao Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Hongera mwalimu Kiarie, kwa kuonyesha mifano Lisanza nikusifie, kwazo sifa nono nono Alwiya zikufikie, ulivyokuwa mfano Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Sikusahau Atonia, kwa wako ukakamavu, Jinsi ulokakania, pasi kuonya ochovu Uneemee dunia, kwa kutupa wangavu Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Wanafunzi mlofika, shukrani nyingi sana Kwenu kuwa washirika, na mwiya wenu kupana Na sisi tukazoeka, na vipindi vil...