Skip to main content

yawezekanaje?

Nomba mkanisikiye, kuna jambo lanikaba
Mbwene linitatiziye, hapa,kwingine ni haba
Yuongoza msimachoye, kama huu sio msiba
Niambiye hala, itawezekanaje?

Yezekanaje nambiye, kipofu yuwaongoza
Wanamfuata wenziye, nyumaye wamfuatiza
Iweje mwe machoye, afuate mja weye jiza?
Niambiye hala, itawezekanaje?

Yuwenda kwenye ndiaye, muendo wa kupapasa
Kawa ategemewaye, insi likuki wamfwasa,
Kama hawapotezeye, na mawi yakawakusa
Niambiye hala itawezekanaje?

Wajenda kimwulizaye, ni kupi pa kukwendea?
Fi kawapa majibuye, ‘lo! Sioni pa kwendea!”
Mjua ndia hijuiye, ije wale wamlungea?
Niambiye hala itawezekanaje?

Hujaona luja aliye, akitoa hata mwengo
Akiita jamaaye, wakatoke zao chengo
“mwizi huyu mbueneye”, wakamfuatiya mgongo
Nambiye hala, itawezekanaje?

Mwizi kufata mwenziye, kuzifuata nyendoze
Ameishika simeye, haja ni akamkomeze
Wanyofu wafuatiye, na luja yuwaongoze,
Nambiye hala, itawezekanaje?

Boza kawa ajuaye, akayashika madaraka
Mwamuzi kawa ni yeye, mwe’enzi na mamulaka
I’je asejua naye, maarifa kuyaweka
Nambiye hala, itawezekanaje?

Mbona asejua naye, asijue asolijua
Ataijua haliye, akawa wakuamua?
Japo yuwadai yeye, utumwa kajifungua
Nambiye hala, itawezekanaje?

Sasa sema nijibiye, nyama mekufungiya
Pali na asejuaye, hajui hajifahamiya
Naye insi ajuaye, hajui achojijuiya!
Nambiye hala, itawezekanaje? 

Comments

Popular posts from this blog

Mja hafi kupenda

Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Yupi mwenye haki

1.           Yupi ale mahuluki, asiye kuwa na doa Ni yupi ale na haki, asiye wa kukosoa Mja ambaye hakiuki, akawa wa kupotea Hayupo muenye haki, maki wote meondoa 2.           Yupi asiye wa kosa, mnyofu wazo nyendo, Awapo aseme sasa, akajinegee kando, Yule ale jitakasa, safi hanao uvundo Hakuna asiyekosa, kwa kauli na matendo 3.           Sijaona aliyejitosha, akahimili nafsiye Insi asejikunguisha, ulimi kwa kauliye Nani asiye keresha, kubughudhi muumbaye Ila tu akajikosha, akatubia dhambiye 4.           Nani asiyekunguwaa, kwa fikra ya moyoni Kunaye asiye na waa, lilofichama wazoni? Awe mja anayefaa, kwa Rabana machoni? Wote wamepunguwaa, utukufu hawaoni.   5.           Yupi basi wa kupona? amchaye Mola wake Nani ataka...