Skip to main content

Bin-Adamu

Mimi
Natakadamu ino nudhumu
Nikayaambe yalomuhimu
Yanotaja ghilba za bin-Adamu
Wa kuhalalisha yalokharamu
kufaidi yake tamaa na hamumu
Yalo mema kayatiya sumu

Na
kuwaseta walomaamumu
Wakijigeuza sanamu
Wakisahau wali wanadamu
Kataka ibada kwa kaumu

Wadhani
Takwepa luhdi wakisha humu
Watakinza ya Mungu Kalamu
Kwamba Muhuluku hafahamu
ati hiyeyuki fuadi ngumu

Ila
Wendelepi siku ya hukumu?
Watapokwima mbele ya Hakimu
Kulipiya wao udhalimu
Kama si nyoto za Jehanamu?
Zitakao waunguza kwa zamu
Zikisha lamba mifupa na damu
Watauma zanda na kujilaumu
kwa wao utimamu wa wazimu

©Wamalwa

Comments

Popular posts from this blog

Ukila

Ukila kile kichakwe, cha mwenzio usile Ukila wa pupa ‘siwe, pupa nayo ni ndwele Ukila haramu s’tukue, cha mwendo sikitwale Ukila nla halali ‘we, cha chira na usile Usile waja kuamba, ‘kawa kauli nawe Usile ukajigamba, kukila kisichakwe Usile na kwa mafamba, litoe jasho lakwe Usile wala kuramba, na cha hila kisiliwe Kisiliwe cha litima, wasio na uwezo Kisiliwe cha yatima, chao wastahilizo Kisiliwe hata kama, wewe una uwezo Kisiliwe na cha umma, tatapika ulazo Ulazo na kwa ghiliba, huwa sumu mwenzangu, Ulazo na ukashiba, utalipa kwa Mungu Ulazo ziwezo baba, fedha za mwendo chungu Ulazo hata zi’haba, ziwe zako ndu’yangu

Kukrani!

Shukrani! Shukrani zangu jazila, kwa chama cha NCOLTCL (nikotiko) Akawajazi jaala, kwa kutupa mualiko Tumeteremea kulla, tulosoma toka kwako Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Sikomi kuwahongera, walimu walofundisha walivyojifunga nira, ya maarifa kutupasha Tuzijenge mbinu bora, Kiswahili kufundisha Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Mambo hayo ni muhimu, mlotupasha uchao Mliyeshusha magumu, ya nadharia zao Tuboreke walimu, kwa wale tufudnishao Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Hongera mwalimu Kiarie, kwa kuonyesha mifano Lisanza nikusifie, kwazo sifa nono nono Alwiya zikufikie, ulivyokuwa mfano Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Sikusahau Atonia, kwa wako ukakamavu, Jinsi ulokakania, pasi kuonya ochovu Uneemee dunia, kwa kutupa wangavu Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Wanafunzi mlofika, shukrani nyingi sana Kwenu kuwa washirika, na mwiya wenu kupana Na sisi tukazoeka, na vipindi vil...