Skip to main content

Popular posts from this blog

Hajafua Dafu Kama alivyo msasi, endaye kuwinda huwa Jenda kwa hamu na kasi,  kilenga kunasa njiwa Zimpatapo khasaisi, kumbe ndege hakutuwa Bado dafu hajafuwa, Mdavadi kijita Mesi Kwa makeke kahujuru, kuitafuta muruwa, Aionje hewa huru, kumbe nako  haikuwa Akapunjwa na Uhuru, alotaka kahiniwa Kabaki mechachamuwa,   zimwishiye furufuru Lisadiki sakumbimbi, walomlisha vongono  Kapotoshwa na wachimbi, na waja wasimaono Kamtowa kwenye kambi, alikopata usono Sasa yuasaga meno, akiulizwa haambi Kendea virambaramba, vichicha vya ukoloni Ndio navyo yuagamba, kuwa farasi mbioni Ni kama guo la mtumba, ‘pambwe mwari arusini Hata hawiki mjini, KANU jogoo wa shamba Nakoma wasiniambe, wanitusi wajuao Nachelea wanichimbe, wan’dhuru vibarakao Ila n’metowa ujumbe, wamwindhe nahodha wao “Sijetuwa meli yao, kwenye kaburi chimbe K.W Wamalwa Mlokole Mlumbi Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison

Ukila

Ukila kile kichakwe, cha mwenzio usile Ukila wa pupa ‘siwe, pupa nayo ni ndwele Ukila haramu s’tukue, cha mwendo sikitwale Ukila nla halali ‘we, cha chira na usile Usile waja kuamba, ‘kawa kauli nawe Usile ukajigamba, kukila kisichakwe Usile na kwa mafamba, litoe jasho lakwe Usile wala kuramba, na cha hila kisiliwe Kisiliwe cha litima, wasio na uwezo Kisiliwe cha yatima, chao wastahilizo Kisiliwe hata kama, wewe una uwezo Kisiliwe na cha umma, tatapika ulazo Ulazo na kwa ghiliba, huwa sumu mwenzangu, Ulazo na ukashiba, utalipa kwa Mungu Ulazo ziwezo baba, fedha za mwendo chungu Ulazo hata zi’haba, ziwe zako ndu’yangu

Mwana nakuasa

Leo nimekuita mwana, Nikupe yangu ya moyo Kwa upole nitanena ‘Kayatiye masikiyo Tabiya hii yako mwana Si yetu tujuwayo Uli wa kulaza damu Na uzembe uzidiyo Pahala nawe hudumu Uchao ni mbiyombiyo Hutufai nawe humu Na hiyo shambiroyo Wapendani naumi Unaiizia gange Hulimi na walimi Wataka ukajitenge Haya sijaona mimi Nakuasa ujichunge Mwiza kazi yu wa chira Ni aendewaye tenge Asiyetaka ajira Wala hashiki shilange Ndiye muja wa hasara Hubomoa asijenge Unavitaka vya bure Hulitoi jasho lako Lako ndizo hamrere Umebaki wa mitiko Uchao ‘wa’tuza bure Sizo zetu nyendo zako La mno lako ni ung’are Uzirembe nyele zako Uturi ujirashire Ukatembee kwa deko Hukosi kuzua ghere Na marashi ya mnuko Unazani utaoa? Utamwoa wa nani? Jasho nalo hujatoa, Utachokishika nini? Utaithibiti ndoa? Wa kukubali nani? Unafaa kujitoa, Fanye kazi kwa manani Na mali ukayazoa Hamadi kibindoni Ndipo utapopoa Ukamtafute mwendani Si mambo ya kutanga Fi na huyu fi na ...