Skip to main content

sipendi kupayuka

Sikupendi kupayuka,
ila leo ninatamka
Mlokole n'tasikika,
bure sipendi 'payuka

Mtima ukisalitika,
kusema utataka
ukaweze kusikika,
bure sipendi payuka

Ni huba limeuteka,
kawa umesalitika
bakunja limeuteka
bure sipendi payuka

Ndio kunadi 'kataka
kote wanikasikika
mie men'teka haraka
bure sipendi payuka

Comments

Popular posts from this blog

Ningekwambia!

Kama ingekuwa vile, swahiba ningeshasema Ningepiga na kelele, ufahamu himahima Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima Ningejasiri n’kwambie, lau sikupendi mbuya Kama sivyo ‘ngekwambiya, wazi wazi pasi siri Lau sijasuhubiya, nahari sikufikiri Kwamba sijakuwaziya, na gonezi kuabiri Ngaungama wangu mwari, kwamba siwe nimpendaye Kama kuli mwengineye, ninaye muenendea Mtimangu anitwaliye, ni radhi kumwenendea Hadhi yangu nimpaye, na siwe wangu maridia Ngakwambia siweye, hala ningekuhubiri Kama siwe ulinitwaa, kawa wa kunipa tuo Najenenda nili fwaa, nimetekwa na pumbao Azizi u’vyonivaa, yakaniisha matao Kweli ningeshakujuza, kwamba siwe nyonda

Mwana nakuasa

Leo nimekuita mwana, Nikupe yangu ya moyo Kwa upole nitanena ‘Kayatiye masikiyo Tabiya hii yako mwana Si yetu tujuwayo Uli wa kulaza damu Na uzembe uzidiyo Pahala nawe hudumu Uchao ni mbiyombiyo Hutufai nawe humu Na hiyo shambiroyo Wapendani naumi Unaiizia gange Hulimi na walimi Wataka ukajitenge Haya sijaona mimi Nakuasa ujichunge Mwiza kazi yu wa chira Ni aendewaye tenge Asiyetaka ajira Wala hashiki shilange Ndiye muja wa hasara Hubomoa asijenge Unavitaka vya bure Hulitoi jasho lako Lako ndizo hamrere Umebaki wa mitiko Uchao ‘wa’tuza bure Sizo zetu nyendo zako La mno lako ni ung’are Uzirembe nyele zako Uturi ujirashire Ukatembee kwa deko Hukosi kuzua ghere Na marashi ya mnuko Unazani utaoa? Utamwoa wa nani? Jasho nalo hujatoa, Utachokishika nini? Utaithibiti ndoa? Wa kukubali nani? Unafaa kujitoa, Fanye kazi kwa manani Na mali ukayazoa Hamadi kibindoni Ndipo utapopoa Ukamtafute mwendani S...

Raha ina karaha

Nisikiye muandani, hili langu ‘takufaa Likulinde maishani, upate na manufaa Usikimbilie rahani, si kwote kwa shufaa Raha siyo ya furaha, mbambonimwe mna karaha Raha haiji kisolo, huja imepachana Unalodhania silo, huwa limepindana Unapolipata hilo, na jingine wakutana Siirambitie raha, mbambonimwe mna karaha Maumbile yakufunze, yana mfano murua Kwanza mulima uanze, pindi bonde tagundua Au mchana na nuruze, usiku utazipindua Ukisha icheza zeze, simile kwaja simanzi Husikii usesikiya, upate na uelewa Wazee ‘lijisemeya, ja bakuli na kawa Raha ukifurahiya, karaha hitachelewa Mwana  ukaindhari, baada ya raha karaha Uchovyapo na asali, usiwe mwenye pupa sana Na utamu wa asali, kuna nyuki na usena Sasa uki si wa azali, una sumu ya usena Na dunia k’ikumbata, kajikaliye yahiyatu Tamati nimeifika, sina mengi ya kunena Sipende kukaramka, ukakosa indhana Raha simfanye kaka, rafiki wa kupendana Mbona usena wa nyuki, nao huo si usena?