Skip to main content

Asiye nacho hanacho

Asiye nacho hanacho, hanacho cha kutaja,
Kutaja kiitikacho, kiitikacho na mkikaja
Kikaja na kilicho, kilicho chenye faraja
Faraja tu hanacho, hanacho huyo mja
Mja wa kicho hanacho, hanacho ila ana Ja’

Jalali mwenye jaala, jaala ilo ya kheri,
Kheri njema na fadhila, fadhila na mstakabali,
Mstakabali uso dhila, dhila wala nayo shari,
Shari amemkomela, amemkomela dahari
Dahari amemfadhila, amemfadhila Jabari

Jabari urithi wake, wake yule fakiri
Fakiri basi simcheke, simcheke na ghururi,
Ghururi haifai kwake, kwake japo hakung’ari,
Hakung’ari na vyake, vyake vilivyo dhahiri,
Dhahiri usimcheke, usimcheke upate shari,

Shari takuta fulani, fulani msahaulifu,
Msahulifu wa kanuni, kanuni na wadilifu
Wadilifu wa Manani, Manani mwenye kukifu,
Kukifu akakuhini, akakuhini mpujufu,
Mpujufu msihisani, hisani kwa wapungufu

Wapungufu si wa moyo, moyo wanao tele,
Tele imani wanayo, wanayo na simile,
Simile iwongozayo, iwongozayo milele
Milele ‘na kimbiliyo, kimbiliyo la waele
Waele siha hawayo, hawayo japo ndwele,

Ndwele yake aijua, aijuaye Rabana
Rabana atamwinua, atamwinua ukiona
Ukiona utang’amua, utang’amua maana
Maana utatambua, utatambua japo hana
Hana chake twajua, twajua ana Rabana

Comments

Popular posts from this blog

uketo wa sanaa ya ushairi

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Ningekwambia!

Kama ingekuwa vile, swahiba ningeshasema Ningepiga na kelele, ufahamu himahima Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima Ningejasiri n’kwambie, lau sikupendi mbuya Kama sivyo ‘ngekwambiya, wazi wazi pasi siri Lau sijasuhubiya, nahari sikufikiri Kwamba sijakuwaziya, na gonezi kuabiri Ngaungama wangu mwari, kwamba siwe nimpendaye Kama kuli mwengineye, ninaye muenendea Mtimangu anitwaliye, ni radhi kumwenendea Hadhi yangu nimpaye, na siwe wangu maridia Ngakwambia siweye, hala ningekuhubiri Kama siwe ulinitwaa, kawa wa kunipa tuo Najenenda nili fwaa, nimetekwa na pumbao Azizi u’vyonivaa, yakaniisha matao Kweli ningeshakujuza, kwamba siwe nyonda