Skip to main content

Mchunguze vizuri



Leo tamwona mwovu, amenawiri
Apataye kwa kiwavu,ndiye tajiri
Nawe uliye mnyovu, unayo shari
Chunga sikwingiye wivu, wewe subiri
Ajitendaye manguvu, na takaburi
Mchunguze vizuri

Kesho iatakudhihiri, ametoweka
Mtu yule aliyejibari, katononoka
Yamemkuta ya shari, ‘kaporomoka
Utafute kwa indhari, nayo hakika
Hutomwona nayo kheri, ameondoka
Mchunguze vizuri
 
Miye huyu nakweleze, yalo ya kweli
Zimefupishwa sikuze,haendi mbali
Mola ajua insize, k’watajamali
Ampa njema sikuze, mustakabali
Mwovu mali si malize, muhifadhili
Mchunguze vizuri

Asema wazi mwenyezi, kitabunimwe
Mjawe kumwacha hawezi, hatupwi kamwe
Waovu tawaweka wazi, shetani pamwe
Na wanyofu awajazi, wahifadhiwe
Wovu wadhili kwa kazi, wakufaidiwe
Mchunguze vizuri

Comments

Popular posts from this blog

uketo wa sanaa ya ushairi

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Ningekwambia!

Kama ingekuwa vile, swahiba ningeshasema Ningepiga na kelele, ufahamu himahima Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima Ningejasiri n’kwambie, lau sikupendi mbuya Kama sivyo ‘ngekwambiya, wazi wazi pasi siri Lau sijasuhubiya, nahari sikufikiri Kwamba sijakuwaziya, na gonezi kuabiri Ngaungama wangu mwari, kwamba siwe nimpendaye Kama kuli mwengineye, ninaye muenendea Mtimangu anitwaliye, ni radhi kumwenendea Hadhi yangu nimpaye, na siwe wangu maridia Ngakwambia siweye, hala ningekuhubiri Kama siwe ulinitwaa, kawa wa kunipa tuo Najenenda nili fwaa, nimetekwa na pumbao Azizi u’vyonivaa, yakaniisha matao Kweli ningeshakujuza, kwamba siwe nyonda