Skip to main content

Tulikotoka!(limetafsiwa)

Huko tulikotoka!!
Japo hakuna umbo wala sura
Lakini kulituunda na kutupa sura
Japo wengi walilemazwa na kuachwa vichwara
Waliofahamu ngomani walisowera
Na umbali huu wajisukuma
Japo huenda kusizue tamaa
Na wengi waweza kupuuza
Lakini twakuonea fahari tunavyoweza
Tukijua  kumetupa na jina
Tulitoa machozi na bila raghba
Sasa twavuna naima tukiimba
Na hivyo tunamwadhimisha Yeye
Aliyetutia nguvu japo wanyonge tuwiliye
Sasa twakuonea fahari tulikotoka!!

Rejea, tazama na usailie
Utaona hakuna kitu ukifurahie
Na ukute kuwa hapana kitu kiwilie
Ulitima wake ulishamirie
Nusura kinamasini tuzamie
Lakini hatukutamauka tusishikilie
Kwa tumaini la ng’ambo litusubirie
Tukaipuuza njaa ilishadidie
Kwani nyoyo na nafsi zetu zilipanie
Wala zisitamauke na pale ziangukie.
Tumaini! Tumaini ndo nanga ilitushikilie
Tumaini la kesho itutadhayalie
….Na leo! Twatazama jana toka hapa tufikie
Twakutabasamia kwa fahari tulikotokea

Comments

Popular posts from this blog

uketo wa sanaa ya ushairi

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Ningekwambia!

Kama ingekuwa vile, swahiba ningeshasema Ningepiga na kelele, ufahamu himahima Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima Ningejasiri n’kwambie, lau sikupendi mbuya Kama sivyo ‘ngekwambiya, wazi wazi pasi siri Lau sijasuhubiya, nahari sikufikiri Kwamba sijakuwaziya, na gonezi kuabiri Ngaungama wangu mwari, kwamba siwe nimpendaye Kama kuli mwengineye, ninaye muenendea Mtimangu anitwaliye, ni radhi kumwenendea Hadhi yangu nimpaye, na siwe wangu maridia Ngakwambia siweye, hala ningekuhubiri Kama siwe ulinitwaa, kawa wa kunipa tuo Najenenda nili fwaa, nimetekwa na pumbao Azizi u’vyonivaa, yakaniisha matao Kweli ningeshakujuza, kwamba siwe nyonda