Skip to main content

Ungejua wafu wamo!



Ugani ninajitoza, kilima mimi kulumba,
Angaa nikakujuza, nikakutoe ushamba,
Lau utajifunza, ili uwache kutamba,
Angejua wafu wamo, na humo kuna kaburi!

Washangaa nasemani,hebu nipe masikivu.
Nikudokolee  jamani, wewe usiye mtuvu,
Wendaye madanguroni, usiye saka wokovu,
Ungejua wafu wamo,na humo kuna kaburi!

Ngejizuia usare, utuwe uhayawani
Ukaukome ukware, ujituze na nyumbani,
Wewe si manoware, wakupenya machakani.
Ungejua wafu wamo, na humo mna kaburi!

Wengi huko wameenda, wakarejea na janga,
Labda hawakupenda! Uliwapeleka ujinga.
Sasa hivi wamekonda, majuto yanawatinga.
Ungejua wafu wamo, na humo muna kaburi!

 Humo muna kaburi, lisiloshibia tumbo,
Lawameza wa kiburi, walojaa jigambo,
 Walovaa takaburi, na kizitanua kumbo
Ugejua wafu wamo, na humo muna kaburi!

Ungeapa walahi, huko guulo hutii.
Moyowo ungenasihi, na kuomba kwa bidii,
Hata usije wahi, wala huko hupitii
Ungejua wafu wamo, na huko kuna kaburi.

Heri mie niondoke,lakini hili jitwalie.
Ukome na ukatike, katu usijililie
Utapobaki pweke ,yeyote asikujilie
Jangalo ulile peke, waja wamekuambaa!

Comments

Popular posts from this blog

uketo wa sanaa ya ushairi

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Ningekwambia!

Kama ingekuwa vile, swahiba ningeshasema Ningepiga na kelele, ufahamu himahima Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima Ningejasiri n’kwambie, lau sikupendi mbuya Kama sivyo ‘ngekwambiya, wazi wazi pasi siri Lau sijasuhubiya, nahari sikufikiri Kwamba sijakuwaziya, na gonezi kuabiri Ngaungama wangu mwari, kwamba siwe nimpendaye Kama kuli mwengineye, ninaye muenendea Mtimangu anitwaliye, ni radhi kumwenendea Hadhi yangu nimpaye, na siwe wangu maridia Ngakwambia siweye, hala ningekuhubiri Kama siwe ulinitwaa, kawa wa kunipa tuo Najenenda nili fwaa, nimetekwa na pumbao Azizi u’vyonivaa, yakaniisha matao Kweli ningeshakujuza, kwamba siwe nyonda