Skip to main content

Raha ina karaha

Nisikiye muandani, hili langu ‘takufaa
Likulinde maishani, upate na manufaa
Usikimbilie rahani, si kwote kwa shufaa
Raha siyo ya furaha, mbambonimwe mna karaha

Raha haiji kisolo, huja imepachana
Unalodhania silo, huwa limepindana
Unapolipata hilo, na jingine wakutana
Siirambitie raha, mbambonimwe mna karaha

Maumbile yakufunze, yana mfano murua
Kwanza mulima uanze, pindi bonde tagundua
Au mchana na nuruze, usiku utazipindua
Ukisha icheza zeze, simile kwaja simanzi

Husikii usesikiya, upate na uelewa
Wazee ‘lijisemeya, ja bakuli na kawa
Raha ukifurahiya, karaha hitachelewa
Mwana  ukaindhari, baada ya raha karaha

Uchovyapo na asali, usiwe mwenye pupa sana
Na utamu wa asali, kuna nyuki na usena
Sasa uki si wa azali, una sumu ya usena
Na dunia k’ikumbata, kajikaliye yahiyatu

Tamati nimeifika, sina mengi ya kunena
Sipende kukaramka, ukakosa indhana
Raha simfanye kaka, rafiki wa kupendana
Mbona usena wa nyuki, nao huo si usena?

Comments

Popular posts from this blog

uketo wa sanaa ya ushairi

Mja hafi kupenda Hapana mja duniani, apenda aondowe Si khiari asilani, rohoye aitowe Aingiye pa gizani, kusiko na mwendowe Maja hafi kupenda, n’ kudura itimiye Ni kudura ya Manani, alompa utuwe Hana na lake Fulani, sema akohowe Hanalo la lakini, zake ziandikiwe Mja hafi kupenda, n’kudura itimiye          Nyaka zikiwa shirini,ni jaala apawe Au aishi theneni, neema ajaliwe Mja hana kwa nini,ikiwa aitiwe Mja hafi kupenda,n’ kudura itimiye Lau ngapewa idhini, k’teuwa atakaye Ngebaki duniani, amwali ajiliye   Afurahi maishani, na wale wampendaye Mja hafi kupenda , n’kudura itimiye

Ningekwambia!

Kama ingekuwa vile, swahiba ningeshasema Ningepiga na kelele, ufahamu himahima Kwamba sikuwazi miye, sikomi laili nzima Ningejasiri n’kwambie, lau sikupendi mbuya Kama sivyo ‘ngekwambiya, wazi wazi pasi siri Lau sijasuhubiya, nahari sikufikiri Kwamba sijakuwaziya, na gonezi kuabiri Ngaungama wangu mwari, kwamba siwe nimpendaye Kama kuli mwengineye, ninaye muenendea Mtimangu anitwaliye, ni radhi kumwenendea Hadhi yangu nimpaye, na siwe wangu maridia Ngakwambia siweye, hala ningekuhubiri Kama siwe ulinitwaa, kawa wa kunipa tuo Najenenda nili fwaa, nimetekwa na pumbao Azizi u’vyonivaa, yakaniisha matao Kweli ningeshakujuza, kwamba siwe nyonda